Job Poa

NACTE: The list of Authorized Institutions to Register new Students (March & April Intake) 2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoundwa kwa Sheria ya Bunge, Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vinavyotoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini.

Jukumu mojawapo la Baraza, ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Kwa muktadha huo, Baraza liliendesha zoezi la uhakiki wa Vyuo vinavyotoa elimu na mafunzo ya ufundi kuanzia tarehe 27 Julai hadi tarehe 6 Septemba, 2017. Lengo kuu lilikuwa ni kuhakiki ubora wa mafunzo yanayotolewa pamoja na kubainisha changamoto zinazovikabili Vyuo hivyo katika utoaji wa mafunzo.

Katika uhakiki huo, Baraza lilibaini kuwa, baadhi ya Vyuo vilikidhi viwango vya ubora kwa mujibu wa taratibu za Baraza. Hata hivyo, baadhi ya Vyuo vilibainika kuwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri ubora wa elimu na mafunzo yanayotolewa. Kufuatia zoezi hilo, Vyuo vyote vilivyobainika kuwa na mapungufu vilitaarifiwa na kutakiwa kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa kabla ya kuendelea na udahili wa wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2018/2019.
Hivyo basi, Baraza linautaarifu umma na waombaji wa nafasi za mafunzo kwa ngazi za Astashahada na Stashahada kwa muhula wa masomo wa Machi/Aprili, 2018 kuomba kwenye Vyuo vilivyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye tangazo hili.

Aidha, Baraza linaelekeza kwamba Vyuo ambavyo havipo kwenye orodha iliyoambatanishwa hapa visidahili wanafunzi katika muhula wa masomo wa Machi/Aprili, 2018 bila kupata kibali cha Baraza kama ilivyoelekezwa.

Pia, Baraza linakumbusha kuwa udahili wa Muhula wa Machi/Aprili, 2018 hauhusishi programu zote za Kada ya Afya na Ualimu.
Kuona orodha ya vyuo vinavyokidhi vigezo bonyeza hapa

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE : 8 Machi, 2018

Source: NACTE Official Website

Related Articles

Serikali yamwaga Kazi katika Halmashauri ya Tanga mjini – Apply now- Ajira Tanzania 2018

(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); Tanga Urban Water Supply and Sanitation Authority (Tanga UWASA) is competitively best utility in the Tanzania Water Sector, supplying clean an( safe water and provides sewerage services in the Tanga City. The Authority with the ISO 9001:2015 certification in quality management systems, i hereby seeking for a relevant qualified and […]

Career Opportunities at The World Vision Tanzania, April 2018

NAFASI ZA KAZI/AJIRA WORLD VISION TANZANIA 2018 AIM Project ManagerReference: 9973-17R17131Location: Africa – Tanzania Town/City: DodomaApplication Deadline Date: 19-Apr-18Category: Health Type: Fixed term, Full-time International Role: No – Only National applicants will be considered.Duration: Less Than 1 YearJOB DESCRIPTIONPurpose of the position:To technical support in improving infant and maternal health through a community based participatory approach on children […]

Ajira Tanzania 2018

Nairobi Hospital Job Vacancy : Senior Registrar- Kenyan Jobs 2018

(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); The Nairobi Hospital, a leading health care institution in Eastern Africa has excellent career opportunities for individuals who possess a passion for excellence, strong work ethic, are results oriented and committed to continual improvement. The successful candidates will be team players with the ability to effectively add value to enabling […]